Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miradi ya Mil. 420 yatekelezwa Kahama

Miradi Ya Mil. 420 Yatekelezwa Kahama Miradi ya Mil. 420 yatekelezwa Kahama

Fri, 27 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 420 imetekelezwa na Serikali ndani ya kata ya Kahama wilayani Ilemela ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, katika umbali mfupi na kwa gharama nafuu.

Hayo yamebainishwa na mtendaji wa kata ya Kahama Ndugu Victor Leonard wakati wa kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Thereza Kahama ambapo amesema kuwa Serikali imejenga shule mpya ya sekondari ya Lubuka, shule mpya ya msingi Kahama, ujenzi wa barabara, mitaro na madaraja mtaa wa magaka na Isela huku barabara ya kutoka Magaka na Kahama zikijengwa kwa kiwango cha Lami.

".. Serikali iko na wananchi wake kuhakikisha miradi mikubwa na midogo ya maendeleo inatekelezwa na Sisi watu wa kahama tumepata fedha nyingi sana katika kipindi hiki kuliko kipindi chochote kufanya maendeleo ..’alisema.

Aidha, Ndugu Victor amewaasa wananchi wa kata hiyo kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli za maendeleo pamoja na kumshukuru Rais wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kutoa fedha za maendeleo, Mbunge Dkt Angeline Mabula apongezwe kwa namna anavyosimamia fedha hizo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM kata ya Kahama Ndugu Mathayo Nicholaus Jibumbile mbali na kuipokea taarifa hiyo amepongeza utekelezaji wa maendeleo ndani ya kata yake pamoja na kuwataka wenyeviti wa mitaa kuhakikisha wanahamasisha jamii kupeleka watoto shule ili fedha za ujenzi wa madarasa zilizotolewa na Serikali ziwe na tija.

Diwani wa kata ya Kahama Mhe Samuel Masune Shimbe amewataka wananchi kuwa wavumilivu kutokana na kero ya ukosefu wa huduma ya uhakika ya maji kwani Serikali imeshachukua hatua kumaliza kero hiyo kwa kujenga tanki kubwa la maji jirani na ofisi za mkuu wa wilaya ya Ilemela mradi uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni sita mpaka kukamilika kwake.

Akihitimisha kikao hicho, Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela kanda ya Buswelu Bi Julieth Peter amewataka wananchi kuhakikisha wanatumia fursa za kiuchumi zinazowazunguka ikiwemo mafunzo ya kilimo yanayotolewa na Serikali bila malipo na mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani inayotolewa na halmashauri zote nchini bila riba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live