Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Milioni 598 kujenga barabara Kawe

Pesa Fedhaddd Milioni 598 kujenga barabara Kawe

Wed, 31 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeanza kutoa fedha za dharura kwa ajili ya ukarabati wa barabara mbalimbali zilizoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha ili kuwezesha shughuli za wananchi kuendelea.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Deogratius Ndejembi leo Januari 31 wakati kipindi cha maswali na majibu katika Mkutano wa Kumi Na Nne.

Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima alietaka kujua serikali ina mpango gani wa dharura kurejesha miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini ikiwamo katika jimbo lake.

Naibu Waziri Ndejembi amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) imeanza kutoa fedha za dharura kurejesha miundombinu ya barabara nchini na katika jimbo la Kawe, Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 598/- imepelekwa kwa ajili ya kufungua barabara na kuanza kupitika pamoja na maeneo mengine nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live