Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mila ya ‘kumaliza msiba’ inavyowatesa wanawake Mara

Mila Mila.jpeg Mila ya ‘kumaliza msiba’ inavyowatesa wanawake Mara

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: Mwananchi

Mila ya ‘kumaliza msiba’ ni miongoni mwa mila kandamizi zinazoendelea katika baadhi ya makabila mkoani Mara inayotweza utu wa mwanamke anayetakiwa kujamiiana na mwanaume yeyote pindi anapofiwa na mumewe kwa madai ya kujisafisha. Baadhi ya makabila yanayotekeleza mila hiyo ni pamoja na Waluo, baadhi ya jamii ya Wakurya, Wajita na makabila mengine ndani ya Mkoa wa Mara yakiamini isipofanyika marehemu atamsumbua mkewe pamoja na ukoo kuwa na mikosi. Sophia John, muhanga wa mila hiyo anasema kabla ya matanga kuisha wazee wa ukoo hasa kina bibi hutumwa kwa mjane kumueleza kuhusu mila hiyo. Sophia ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Maburi Wilaya ya Serengeti anasema ili kumaliza msiba, mwanamke aliyefiwa na mume analazimika kumtafuta mwanaume wa kujamiiana naye kwa siku moja ikiwa ni ishara ya kutimiza takwa hilo la kimila na baada ya hapo anakuwa huru. Anaeleza jukumu la kumtafuta nwanaume wa kujamiiana naye linakuwa juu ya mwanamke husika, hivyo muda ukifika huenda popote kumtafuta amtakaye. “Sikupata shida nilimtafuta mwanaume nikamweleza nia yangu na kwa sababu ni wa kabila moja alikubali na siku iliyofuata alikuja nyumbani nikalala naye huku wazee wakiwa nje kwa ajili ya kuthibitisha na baada ya hapo maisha yaliendelea kama kawaida," anasema. Sophia anasema kuna wanawake wengine wanapata wakati mgumu kuwapata wanaume wa kutekeleza hilo, hivyo hulazimika kutoa fedha ili wakubali. Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Anna Dishon anasema mwanamke anatakiwa ‘kumaliza msiba’ na mwanaume aliyempata mara moja pekee na endapo watarudia, mwanaume huyo anapatwa na jambo baya ikiwamo kufariki dunia. “Hii mila ingawa inalenga kumaliza msiba wa mume, lakini kuna utofauti kidogo katika kuitekeleza. Mfano kuna wengine unatakiwa kumleta nyumbani kwako mwanaume uliyempata na kulala naye ili wana ukoo wawe na uhakika umetekeleza, lakini wengine wanatakiwa kulala naye hukohuko kisha kurudi nyumbani kuleta taarifa,”anasema Anna. Licha ya kuwepo kwa mapambano dhidi ya mila zisizofaa ikiwemo hiyo, anasema bado inatekelezwa kwa kiasi kikubwa hasa maeneo ya vijijini. Jambo la kusikitisha zaidi, anasema hivi sasa wanawake wengi wanalazimika kuwatafuta wanaume wenye matatizo ya akili au walevi wa kupindukia ili kuteketeza mila hiyo kwa sababu wanaume wengine wanakataa. “Kuna dhana kuwa wanaume wanaokubali baada ya hapo nao hufariki dunia au kurukwa na akili wakienda kushiriki tendo la ndoa na wake zao. Pia ni vigumu mwanamke kumtongoza mwanume hadi akubali kwa hiyo wanaona bora watafute wenye matatizo ya akili au walevi,” anasema. Anaeleza alipofiwa na mumewe alikuwa na mtoto mchanga, hivyo ukoo ulimsubiri hadi alipomuachisha mtoto kunyonya kisha akatakiwa kumaliza kuifanya mila hiyo. “Nilimyonyesha mtoto kwa miaka miwili na nilipomuachisha tu nikaambiwa natakiwa kumaliza msiba, sikuwa na namna nikamtafuta mwanaume tukakubaliana na baada ya hapo kila mtu akaendelea na maisha yake,” anaeleza. Mary Walter, anasema mila hiyo ni mateso kwa wanawake, kwani upo uwezekano wa kutengwa na jamii akikataa. Anasema alijifungua mwezi mmoja baada ya kifo cha mumewe na alinyonyesha kwa zaidi ya mwaka mmoja, ndipo baba mkwe wake alipoanza kumfanyia fujo akitaka afanye mila hiyo. Anasema watu wanaamini endapo haitafanyika, laana itaikumba familia na ukoo mzima. Mary anasema mwanamke anayegoma kumaliza ‘msiba wa mumewe’ kwa njia hiyo hutengwa na jamii na haruhusiwi kukanyaga shamba la mtu yeyote wala kwenda sokoni au kwenye mkusanyiko ya watu kwa ajili ya shughuli za kijamii. “Na ikitokea ukafiwa na ndugu wakati haujamaliza msiba wa mumeo hauruhusiwi kulia na kutoa machozi na endapo una binti anataka kuolewa wachumba hawataruhusiwa kuja kuchumbia maana mji wako unadaiwa una mikosi," anasema. ...Sina taarifa, ni hatari kiafya Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka anasema hana taarifa ya uwepo wa mila hiyo, lakini akatoa wito kwa wananchi kuachana nayo kwani haina manufaa. Chikoka anasema mila hiyo ni hatari kiafya kwani wanawake wanalazimika kutafuta wanaume wasiowajua na kujamiiana nao, jambo linaloweza kusababisha kupata maambukizi ya magonjwa ikiwemo Ukimwi. Mwanaharakati wa haki za wanawake, Rhobi Samuel, anahoji, "kama hii mila ni nzuri kwanini wanaotakiwa kuitekeleza ni wanawake tu, kwanini wanaume nao wanapofiwa na wake zao nao pia wasifanye hivyo? Suala la ustawi wa jamii si linahusu jinsia zote?" Anasema kitendo cha kumtaka mwanamke kwenda kumtafuta mwanaume yoyote wa kujamiiana naye sio jambo la busara na linashusha utu wa mwanamke. Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mara, Neema Ibamba anasema Serikali inatambua uwepo wa mila hiyo na wamekuwa wakishirikiana na wadau kutoa elimu juu ya madhara yake.

Chanzo: Mwananchi