Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mil 451 /- zatengwa kumaliza tatizo la umeme Mpwapwa

4b4598df5bf790d856ad2041f6a92656 Mil 451 /- zatengwa kumaliza tatizo la umeme Mpwapwa

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21 limetenga Sh 451 milioni kwa ajili ya kumaliza tatizo la kukatika katika kwa umeme katika wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma.

Meneja wa TANESCO wilayani hapa, William Njovu aliyasema hayo katika kikao cha madiwani alipokuwa akitoa taarifa yake ya usambazaji wa umeme katika mji huo.

Njovu alisema Mpwapwa ina vijiji 113 kati ya vijiji hivyo 80 vina huduma za umeme na vijiji 33 vilivyosalia vitaunganishwa huduma hiyo katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Njovu alisema Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya zinazokabiliwa na changamoto ya kukatikakatika kwa umeme ambako alisema kunasababishwa na umbali uliopo kati ya kituo kikuu cha Zuzu, wilayani Dodoma na wilaya hiyo.

Alisema changamoto kubwa ya kukatika katika kwa umeme ni urefu wa njia ambapo ni zaidi ya kilomita 200

na jiografia ya wilaya ya Mpwapwa na uchakavu wa miundombinu.

Hata hivyo alisema, wanajenga kituo kidogo Mtera cha kupunguza umbali na ujenzi wake unaendelea na kitakamilika muda si mrefu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa, George Fuime aliutaka uongozi wa shirika hilo kujipanga na kupunguza tatizo hilo ambalo limekuwa kikwazo cha maendeleo katika mji wa Mpwapwa.

Naye Diwani wa Viti Maalumu, Mery Kaguli (CCM) alisema hali ya kukatikakatika kwa umeme katika mji huo kunaweza kusababisha maafa.

Chanzo: habarileo.co.tz