Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikopo nje nje kwa vijana wanaojihusisha na Samaki Kawe

Ca29cdc8376911da2faea0258d3d9b73.jpeg Mikopo nje nje kwa vijana wanaojihusisha na Samaki Kawe

Mon, 7 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewashauri Vijana wa Jimbo la Kawe mkoani Dar es Salaam kuunda vikundi ili kufaidi fursa mbalimbali za mikopo zinazotolewa na wizara hiyo.

Kauli hiyo ameitoa Bungeni hapa leo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima (CCM) aliyetaka kujua ni lini serikali itaanza kutoa mikopo kwa vijana wengi wanaovua kwa kutumia mitumbwi midogo katika Bahari ya Hindi?

Naibu Waziri Ulega amesema, vijana wa jimbo hilo wanatakiwa kujiunda katika vikundi ili kupata mikopo inayotolewa na wizara hiyo ikiwemo ya kumununua mashine za boti za uvuvi.

"Pia wanaweza kujiunga katika vikundi ili kupata mikopo ya kutengeneza vichanja vya kukaushia samaki pamoja na kukopa mikopo kwa ajili ya kuzalisha barafu ya kuhifadhia samaki na pia kuwauzia vijana wengine," amesema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz