Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Innocent Bashungwa ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa mingine nchini kufuata utaratibu wa kuanzishwa madawati ya huduma kwa Wateja (One Stop Center) Ili kuweza kuwasaidia wananchi kutatua kero walizonazo.
Waziri Bashungwa alisema hayo leo alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kushuhudia kuwepo kwa Kituo Cha Pamoja Cha kutoa huduma kwa wananchi Mkoani hapa ambapo alitembelea akiwa katika ziara yake ya siku moja.
"Nampongeza sana Mkuuwa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge huku nikielekeza jambo hili ambalo nimeliona hapa Mkoa wa Pwani liigwe na kutekeleza Wakuu wa Mikoa mingine kote nchini kwa kufuata utaratibu huu wananchi watapata utatuzi wa kupata huduma wanazozihitaji ikiwa ni pamoja na kupata utatuzi wa changamoto wanazozipitia hivyo kuwa na vituo vya kutoa huduma kama DASCO, TANESCO,TRA, RITA, UHAMIAJI na huduma nyingine ndani ya Mkoa husika ni muhimu " alisema Mheshimiwa Bashungwa.
Waziri Bashungwa akiwa katika ziara hiyo ndani ya Mkoa wa Pwani alitembelea miradi inayoendeshwa na Shirika la Elimu Kibaha ambalo liliasisiwa mwaka 1963 chini ya Uongozi wa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Julius Kambarege Nyerere kwa kupitia Chama Cha Cha Mapinduzi (CCM) huku lengo la kuanzishwa kwa Tasisi hyio ikiwa ni kupambana na adui ujinga , maradhi na umasikini.
Akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo ameutaka
Uongozi wa Shirika la Elimu Kibaha kujiitathmini katika kuelekea miaka 60 ijayo huku akisema wajipange na kuweka mikakati ya kukua kiuvhumi tofauti na ilivyo sasa.
"Angalizo ninalowapa leo Shirika la Elimu Kibaha angalieni mulekeo wenu kiuchumi, kuweni wabunifu wa miradi endelevu ambayo itawakuza na kuwapaisha Kitaifa fuateni nia na madhumuni kama jinsi alivyoanzisha Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hili Shirika liko Kibaha lakini limebeba sura ya Taifa hivyo kaeni kama timu na mjipange mnaisaidiaje nchi kukua zaidi" alisema Bashungwa.
"Angalieni vijana wanahitimu elimu katika ngazi ya kidato cha nne ambao hawendelei kwenye mfumo wa kuendelea na elimu ya juu hivyo angalieni namna gani mnawasaidia , Shirika la Elimu Kibaha linakua ni wajibu wenu kuwajengea uwezo vijana ambao huishia njiani kadhalika hata wahitimu wa elimu ya juu bado wanahitaji ninyi muwasaidie na kuisaidia serikali, andikeni mradi TAMISEMI tupo tutawasimamia kufanikisha ninyi ni Shirika la Elimu la Kitaifa kuweni makini" alisema Bashungwa.
"Ninyi hamna hoja mahsusi binafsi nilitegemea kuja kuona miradi mikubwa hapa tofauti na nilivyoona ni miradi ambayo imekuwa ya kawaida na inayofanyika katikamaeneo mengine kama jinsi nilivyoona ujenzi wa shule za awali madarasa hapa ninyi kama Taasisi mnatakiwa muhame huku mkapambane na adui umasikini,
anzisheni miradi mikubwa ya kilimo kwa mashamba ya 'Green House' kwa kulima mazo kama maparachichi na kuuza nje ya nchi nasema haya sababu Mkoa wa Pwani uko jirani na Jiji la biashara Dar es Salaam hivyo mnapaswa muamke mshirikiane na vyuo kama Veta, Sido, Camatec endapo mkiunganisha nguvu na kukusanya vijana mtachangia kupambana na umasikini nchini na kuzalisha ajira kwa vijana" alisema Bashungwa.
Katika ziara hiyo Waziri Bashungwa pia aliangalia fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya elimu, Kama zinaendana na thamani ya pesa iliyotolewa na kuridhishwa na miradi hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa kupitia fedha zilizotolewa na serikali lakini pia ukarabati wa shule kongwe ya ya wavula ya Kibaha sekondari.
Mbali ya ujenzi wa miundo mbinu ya elimu inayoendelea nchi nzima ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa, Waziri Bashungwa amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa walimu hivyo ina mpango wa kuhakikisha inajenga nyumba za walimu na kumaliza changamoto zao kwa kushirikiana na chama cha Walimu CWT.