Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikoa minane kusini Tanzania yashirikiana kutangaza utalii

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbozi. Katika kuunganisha nguvu za kutangaza utalii wa kanda ya kusini, mikoa minane ya Tanzania imeshiriki maadhimisho ya siku ya kimondo duniani yanayofanyika Julai Mosi kila mwaka.

Baada ya mafanikio ya utalii katika mikoa ya kaskazini yaliyochangia kutambulika kwa Hifadhi ya Taifa Serengeti kunyakua tuzo ya hifadhio bora zaidi Afrika mwaka 2018, juhudi zaidi zinaelekezwa kusini kuwainua wananchi na vivutio walivyonavyo.

Kuanza utekelezaji wa mkakati huo, katibu mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda amesema tayari wakuu wa mikoa hiyo wamekubaliana na Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Morogoro imewakilishwa mwaka huu.

“Mikoa yote imeshiriki maadhimisho ya siku ya mwaka 2019, ushirikiano huo utaendelea katika vivutio vya mikoa mingine,” amesema Profesa Mkenda.

Katibu tawala mkoa wa Katavi, Abdala Malela amesema ushirikiano huo utasaidia kuhamasisha utalii wa ndani na nje kwa kuwaeleza wananchi vivutio vilivyopo kama vile maporomoko ya Kalambo yaliyopo mkoani Rukwa na Hifadhi ya Katavi yenye wanyama wakubwa kuliko zote nchini.

Mkoa wa Morogoro unajumuishwa katika ukanda huo kutokana na hifadhi zake kuanzia kusini.

Pia Soma

Tanzania ni  nchi ya pili kwa wingi wa vivutio lakini mwaka jana ilipokea watalii milioni 1.37 tu ingawa mkakati uliopo ni kufikisha watalii milioni mbili mwakani.

Miongoni mwa juhudi zinazofanywa ni kutangaza vivutio vilivyopo katika nchi za Ulaya, Amerika na Asia. Hivi sasa, wawakilishi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na waongoza watalii wapo nchini China wanakoshiriki maonyesho ya kimataifa ya uchumi na biashara.

Chanzo: mwananchi.co.tz