Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikoa 17 kukosa umeme

Umeme Gizani.jpeg Umeme

Sun, 9 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) limetoa taarifa kwa Wateja wake kwamba leo Jumapili, Oktoba 9, 2022 kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 10:30 jioni na Jumatatu, Oktoba 10, 2022 kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri baadhi ya maeneo yatakosa umeme.

Mikoa ambayo baadhi ya maeneo yatakosa umeme ni Dar Es Salaam, Pwani, Tanga, Arusha, Morogoro, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Njombe, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Mara, Simiyu, Kilimaniaro, Manyara na Songwe.

Sababu ya umeme kukatwa ni kuzimwa kwa laini mbili kubwa za umeme wa kilovoti 220 kutoka Morogoro hadi Kinyerezi na kutoka Morogoro hadi Kidatu ili kuruhusu matengenezo ya uboreshaji wa miundombinu ya have usafirishaji umeme katika kituo cha Msamvu, Morogoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live