Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikataba 41 ya Ujenzi Dar es salaam

AMOS MAKALA Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Amos Makalla

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: MillardAyo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla leo August 10, 2021 ameshuhudia awamu ya kwanza ya utilianaji sahihi wa mikataba 41 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 14.1 kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara za Mkoa wa Dar es salaam na kuwataka Wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha Miradi kwa wakati na kwa kiwango.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa hafla ya utilianaji sahihi mikataba baina ya TARURA na Wakandarasi ambapo amesema mafanikio haya yote ni matokeo ya kazi kubwa na nzuri ya Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Katika utatuzi kero za Wananchi.

RC Makalla amewaelekeza DAWASA, TANROADS, TARURA, TTCL na TANESCO kufanya kazi kwa pamoja ili kuondoa tatizo la miradi kutomalizika kwa wakati kutokana na Taasisi husika kuchelewa kuhamisha miundombinu.

Pamoja na hayo RC Makalla amewaelekeza TANROADS na TARURA kuhakikisha wanasimamia utunzaji wa miundombinu ya Barabara ikiwa ni pamoja na usafi, ukarabati na uwekaji wa vibao vya kuzuia biashara Kwenye eneo la hifadhi ya Barabara.

RC Makalla ameonesha kufurahishwa na ongezeko la bajeti ya Ujenzi wa Barabara Dar es salaam kutoka Shilingi bilioni 25 hadi bilioni 40 na Nchi nzima kufikia Bilion 300.

Chanzo: MillardAyo