Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili ya watoto waliofariki kwa moto yaagwa

Screenshot 20221125 174109 Facebook Miili ya watoto waliofariki kwa moto yaagwa

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miili ya wanafunzi watatu wa shule ya msingi Buhangija, iliyoko Manispaa ya Shinyanga waliopoteza maisha baada ya bweni walilokuwa wamelala kuteketea kwa moto, imeagwa leo Novemba 25, 2022, katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga na kukabidhiwa kwenye familia zao kwa ajili ya mazishi.

Watoto hao walipoteza maisha baada ya bweni walilokuwa wamelala kuteketea kwa moto usiku wa Novemba 23, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema ameongoza zoezi la kuaga miili ya wanafunzi hao.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Charles Ngelela amesema wamesikitishwa na  vifo vya watoto hao huku viongozi wa dini wakatoa neno la faraja kwa wafiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live