Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili ya waliozama mto Mori kuzikwa kesho

Mtumbipiic Miili ya waliozama mto Mori kuzikwa kesho

Wed, 11 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miili ya watu watano waliofariki dunia baada ya mtumbwi kuzama ndani ya mto Mori itagwa na kuzikwa kwa pamoja katika mazishi yatakayofanyika kesho Alhamisi Mei 12, 2022.

Mazishi hayo yatafanyika baada ya miili yote mitano kupatikana baada ya mwili wa mwisho ambao ni wa mtoto wa miaka mitano kupatikana jana jioni na hivyo kuhitimisha kazi ya kutafuta na kuopoa miili hiyo iliyoanza Mei 7, 2022 baada ya mtumbwi kuzama ndani ya mto huo.

Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka amesema kuwa wanafanya vikao na ndugu wa marehemu na watafikia makubaliano ya eneo ambalo miili hiyo itazikwa pamoja.

"Kwa makubaliano ya awali tumekubaliana tutazika miili kwa pamoja kesho na mazishi yatafayika huko huko kijijini kuhusu eneo na taratibu zingine tutajulishana kwa kadri ya maamuzi ya vikao" amesema Chikoka

Akizungumza baada ya kufika katika eneo la tukio, Mbunge wa Jimbo la Rorya, Jafari Chege amesema kuwa Serikali inakwenda kutafuta suluhisho la kudumu juu ya tatizo la usafiri na vivuko katika maeneo ya mto Mori. miili pic

Mbunge wa Jimbo la Rorya, Jafari Chege ( mwenye kofia) akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kowak alipowatembelea kuwapa pole kutokana na vifo vya watu watano vilivyotokana na mtumbwi kuzama ndani ya mto Mori. Picha na Beldina Nyakeke Advertisement

Amesema kuwa kupitia bajeti ya Tarura anakwenda kuongea na Serikali kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa barabara kutoka katika kijiji cha Kowak kuelekea katika daraja ambalo linajengwa kwenye mto huo ili kurahisisha uvukaji wa mto kwa wakazi wa maeneo hayo.

"Kwavile tayari tumeanza ujenzi wa daraja pale kwenye mpaka wa kata hii ya Nyathorogo na Nyaburongo sasa itakuwa ni vigumu kuomba tena pesa kwajaili ya ujenzi wa daraja hapa badala yake tunatoboa barabara kutoka hapa kuelekea kule darajani ili fedha ipo na tunakwenda kufanya mara moja " amesema Chege

Mei 7 mwaka huu asubuhi mtumbwi uliokuwa ukivusha watu kwenda katika kijiji cha Randa kata ya Kigunga kutoka kijiji cha Kowak ulizama majini na kuuwa watu watano huku wengine watano wakinusurika.

Chanzo cha tukio hilo kimeelezwa kuwa ni kukatika kwa kamba iliyokuwa ikitumiwa na mvushaji kuvuta mtumbwi baada ya mtumbwi huo kubeba watu wengi kuliko uwezo wake huku kikitumia kamba ambazo pia zilikuwa zimechoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live