Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili ya viongozi sita wa CCM waliofariki kwa ajali yaagwa Njombe

Miili Ya Waliofariki Kwa Ajali Miili ya viongozi sita wa CCM waliofariki kwa ajali yaagwa Njombe

Sun, 15 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miili ya Viongozi sita wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya Kata katika Wilaya ya Makete Mkoani Njombe waliofariki kwa ajali ya gari Ijumaa October 13,2023 katika eneo la Ndulamo Wilayami humo wakati wakitoka kwenye mkutano wa Mlezi wa CCM Mkoa wa Njombe, imeagwa leo October 15,2023 katika Kata ya Tandala Mkoani humo na mamia ya Wananchi wakiwemo Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.

Miili ya Viongozi sita wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya Kata katika Wilaya ya Makete Mkoani Njombe waliofariki kwa ajali ya gari Ijumaa October 13,2023 katika eneo la Ndulamo Wilayami humo wakati wakitoka kwenye mkutano wa Mlezi wa CCM Mkoa wa Njombe, imeagwa leo October 15,2023 katika Kata ya Tandala Mkoani humo na mamia ya Wananchi wakiwemo Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali. Miili ya Viongozi ambayo imeagwa ni wa Tumaini Mbilinyi Katibu wa CCM Kata ya Tandala, Linus Sanga Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Kata ya Tandala, Ruth Sanga Mwenyekiti wa UWT Kata ya Lupila, Speransia Sanga Katibu wa UWT kata ya Ipepo, Eva Sanga Katibu wa UWT Kata ya Lupila pamoja na Hebron Mbilinyi Katibu Mwenezi wa CCM Tandala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live