Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili ya polisi yaagwa mkoani Njombe

94465 Pic+polisi Miili ya polisi yaagwa mkoani Njombe

Wed, 5 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Njombe. Wananchi kutoka maeneo mbalimbali mkoani Njombe wameshiriki shughuli ya kuaga miili ya polisi watatu waliofariki katika ajali ya gari mkoani humo.

Polisi hao walifariki dunia jana alfajiri Jumatatu Februari 3, 2020 baada ya gari walilokuwa wamepanda kugongana na basi la kampuni ya Sharon.

Akizungumza katika shughuli hiyo leo Jumanne Februari 4, 2020 mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amesema Serikali imepoteza nguvu kazi ya Taifa kwa kuwa askari hao walikuwa na umri mdogo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah  aliwashukuru  wakazi wa Njombe kwa kujitokeza kwa wingi pamoja sambamba na kutoa michango kuhakikisha askari hao wanasafirishwa katika maziko.

Watu mbalimbali walishiriki ibada ya kuaga miili ya askari hao ambao ni Marianus Hamissi, Michael Mwandu na Henry  Soka.

Chanzo: mwananchi.co.tz