Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili waliosombwa na maji yazua taharuki wilayani Serengeti

93811 Maji+pic Miili waliosombwa na maji yazua taharuki wilayani Serengeti

Fri, 31 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Miili ya waliosombwa na maji imezua taharuki wilayani Serengeti kutokana na wananchi kukaa pembeni ya mto na kutaka kuiopoa bila mafanikio.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Januari 30, 2020 ofisa mtendaji wa kata ya Nyansurura, Neema Binagi amesema miili ya watu imeonekana katika mto Nyahende, kwamba huenda walisombwa na maji katika maeneo tofauti.

"Mwili wa mama aliyembeba mwanaye mgongoni ulikuwa juu ya maji na wananchi wamehangaika kuuopoa lakini kasi ya maji ikawashinda. Wakati wanahangaika ukapita mwili wa mwanaume ambao pia walishindwa kuuopoa,” amesema Neema.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Januari 30, 2020  Neema amesema wananchi hao walikuwa wakitafuta mwili wa kijana aliyesombwa na maji jana Januari 29, 2020 wakati akivuka mto huo.

"Wakati wakiendelea kutafuta mwili wa kijana huyo anayedaiwa alikuwa na mwenzake ndio wakaona miili hiyo inapita. Inaonekana mito yote imefurika na watu wanapolazimisha kuvuka wanasombwa na maji,” amesema.

Katibu tawala wilaya ya Serengeti,  Cosmas Qamara amesema huenda watu watano akiwemo mtoto wamekufa kwa kusombwa na maji.

Pia Soma

Advertisement
“Ndio nimefika Nyahende kwenye tukio, kwa kweli mito imejaa sana maji ni mengi, tunaendelea kufuatilia  naomba wananchi wachukue tahadhari kubwa wasipite ndani ya maji wanapokuta mito imejaa," amesisitiza.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz