Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili waliokufa ajalini Geita yatambulika

MAITI YAPOTEA Miili waliokufa ajalini Geita yatambulika

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati miili ya waliopoteza maisha katika ajali iliyotokea Januari 10, 2024 ikihusisha magari manne katika Pori la Akiba la Kigosi wilayani Bukombe mkoani hapa ikitambuliwa, majeruhi wa ajali hiyo wameongezeka kutoka wanane hadi 11.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Deograsia Mkapa akizungumza na Mwananchi kwa simu amewataja waliotambuliwa kuwa ni Shida Yohana aliyekuwa dereva wa lori na Niclous Masha(24) aliyekuwa utingo, wote wakiwa wakazi wa Kahama mkoani Shinyanga.

Mwingine ni Rehema Hassan (30) mkazi wa Jijini Dar es Salaam aliyekuwa kondakta katika basi la Abood na kwamba kwa sasa taratibu za kukabidhi ndugu miili ya wapendwa wao zinaendelea hospitalini hapo.

Kuhusu majeruhi, Dk Mkapa amesema waliopokewa katika hospitali hiyo ni majeruhi 11.

Amesema waliopewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Mkoa wa Geita ni watatu ambao walipata majeraha ya mifupa na kuhitaji upasuajiwa kutumia vyuma, huku wawili wakipelekwa Bugando kupata uchunguzi wa mfumo wa fahamu kwa kuwa wameumia sehemu ya uti wa mgongo.

Mganga mkuu huyo wa Wilaya ametaja waliojeruhiwa kuwa ni Hassan Ally, Adam John(38) Matungwa Joseph, Izack Tangishaka wote wakazi wa Dar es Salaam.

Wengine ni Erasto Herman (18) Mkazi wa Kahama, Awema Said Mkazi wa Mkuranga mkoa wa Pwani, Nickson Edward mkazi wa Kibondo na Mlokozi Joshua mkazi wa Ngara.

Dk Mkapa amesema kwenye ajali hiyo walipokewa pia watoto wawili Maclata Maftaa (3) na Mahad Maftaa (5) ambao ni ndugu na wanaendelea na matibabu hospitalini hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live