Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili 12 kati ya 13 yaopolewa Ziwa victoria

Ajali Ziwa Victoria (600 X 368) Miili 12 kati ya 13 yaopolewa Ziwa victoria

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya miili 12 kati ya 13 ya waliozama ziwa Victoria baada ya mitumbwi miwili kupigwa na dhoruba, imepatikana leo Jumatano 2, 2023.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere, amesema vikosi vya uokoaji kwa kushirikiana na wavuvi na wenyeji eneo hilo wanaendelea kuutafuta mwili mmoja ambao umesalia.

Julai 30, 2023 mitumbwi miwili iliyokuwa imebeba waumini 28 wa Kanisa Takatifu la Mungu wa Kiroho (KTMK), ilizama ziwani ambapo watu 14 waliokolewa na kukimbizwa hospitalini.

Katika tukio hilo ambapo wengi wa waliozama walikuwa ni watoto, na wanafunzi wa Shule ya Msingi Bulomba wilayani Bunda, huku shughuli ya kuwatafuta ikianza Julai 31, 2023 na hadi sasa bado mwili mmoja unaendelea kutafutwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live