Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili 116 ajali ya MV Nyerere yatambuliwa

18686 Pic+miili+yatambuliwa TanzaniaWeb

Sat, 22 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ukerewe. Miili 116 kati ya 151 iliyoopolewa baada ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018 imetambuliwa na ndugu.

Ndugu, jamaa na wananchi wamepiga kambi eneo la bandari ya Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe tangu kazi ya uokoaji ilipoanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 22, mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema Serikali itatoa ubani wa Sh500, 000 kwa familia, kwa kila maiti itakayotambuliwa na kuchukuliwa kwa ajili ya maziko.

Tangu asubuhi leo, miili 30 imeopolewa na kufanya idadi ya miili iliyoopolewa hadi sasa kufikia 166 baada ya mili mingine 136 kuopolewa hadi jana jioni.

Miili yote iliyoopolewa imehifadhiwa katika Kituo cha afya cha Bwisya.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz