Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Migogoro yakwamisha uwekezaji

11563 Migogoro+pic TanzaniaWeb

Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Muleba. Migogoro ya ardhi kati ya wananchi na wawekezaji wa mifugo kwenye vitalu vya ranchi ya Kagoma wilayani hapa Mkoa wa Kagera, imekwamisha ufugaji wa biashara kwa ng’ombe wa nyama na maziwa baada ya maeneo ya malisho kuvamiwa.

Akisoma taarifa mbele ya mkuu wa mkoa wa huo, Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu kwa niaba ya wawekezaji wenzake, Emmanuel Byabusha alisema wananchi waliovamia maeneo wanayomiliki kisheria wanaendesha shughuli za kilimo maeneo ya mabondeni ambayo hutegemewa na mifugo.

Byabusha alisema kuna zaidi ya ng’ombe 13,000 wa nyama na maziwa katika ranchi hiyo, idadi hiyo ingekuwa imeongezeka kama siyo kukwamishwa na migogoro ya ardhi ambayo husababisha mifugo yao kuvamiwa na kujeruhiwa.

Pia, waliiomba Serikali kuwapunguzia kodi wanazolipa kwa kumiliki vitalu huku takriban asilimia 44 ya ardhi hiyo ikiwa imevamiwa na wananchi na kushindwa kupanua uwekezaji wao.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Jenerali Kijuu alisema mgogoro huo wa muda mrefu umeanza kutafutiwa ufumbuzi kwa kupata hekta 60,000 eneo la Mwisa wilayani Missenyi ambazo vitatengwa vitalu vipya. Alisema Serikali inatumia busara zaidi kumaliza mgogoro huo kwa kuwa wananchi waliovamia maeneo hayo ni wengi na utumiaji wowote wa nguvu unaweza kuongeza ukubwa wa tatizo badala ya kuleta ufumbuzi wa kudumu.

Hata hivyo, Jenerali Kijuu alisema haridhiki na kasi ya uwekezaji katika vitalu hivyo ili kukidhi mahitaji ya sera ya viwanda ambavyo vitahitaji maziwa na mifugo kwa ajili ya viwanda vya nyama.

Naye mwenyekiti CCM kata ya Rutoro, Respicius Gasper alisema mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 15, umeathiri maendeleo ya wananchi ambao huishi kwa hofu na hawawezi kupanua shughuli zao za kilimo na kufuga.

Chanzo: mwananchi.co.tz