Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Migogoro ya ardhi imekithiri DSM" - RC Makalla

Rc Makalladd Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa DSM.

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema mkoa huo bado unakabiliwa na tatizo kubwa la migogoro ya ardhi ukilinganisha na kero zingine za wananchi katika eneo hilo.

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 27, 2021, wakati akitoa tathmini ya ziara yake iliyolenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa majimbo mbalimbali ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

Amesema katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero ndani ya jiji hilo, kati ya kero 927 alizosikiliza, kero 345 ni za ardhi, hali ambayo imetoa picha kwamba tatizo hilo ni kubwa katika mkoa huo.

"Migogoro ya ardhi maana yake kuna wamiliki zaidi ya mmoja, mtu kavaamia bila kuwa na nyaraka za umiliki, niseme kuwa tayari nimeshamuandikia barua Waziri Lukuvi kwenda kushughulikia mgogoro mkubwa wa ardhi uliopo chanika, huu ni mgogoro mkubwa kati ya Wilaya ya Ilala na Kisarawe, tuwe wavumilivu" RC Makalla.

Sanjari na hayo, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia na kutoa maelekezo katika miradi mikubwa hasa iliyoanza kutekelezwa katika Serikali ya awamu ya tano, chini ya Hayati Dkt John Magufuli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live