Wilaya Rungwe mkoani Mbeya kwa kushirikiana na wadau wa kilimo wanatarajia kuzalisha miche milioni 1.6 ya mbao, matunda na kivuli ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayotarajiwa kuathiri sehemu kubwa nchini.
Haya yamebainishwa na Afisa Maliasili wa Wilaya hiyo, Castor Makeula, amesema kuwa miche hiyo itagawiwa bure kwa wananchi kwenye sekta binafsi na umma kwa lengo la kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi kupitia biashara ya mbao na matunda.
"Tumeamua kuzalisha miche milioni 1.6 ya aina mbalimbali kama vile matunda, mbao na kivuli ikiwa ni hatua ya kuhifadhi vyanzo vya maji, kilimo na biashara ili kukuza uchumi wa wakazi wa Rungwe sambamba na utunzaji wa mazingira,” Amesema Afisa huyo.
Vile vile, amesema kuwa kwa sasa wanaendelea kuzalisha miche hiyo na ifikapo Januari 2022 wananchi wataanza kugawiwa ka kushirikiana na viongoi wengine Wilayani humo.