Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhanga ajali ya Moto Mkokotoni afunguka (+Video)

Moto Mkokotoni Mhanga ajali ya Moto Mkokotoni afunguka

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mheshimiwa Ayoub Mohammed Mahmoud amesema timu ya wataalamu kutoka kamisheni ya Maafa Wilaya ya kaskazini A inaendelea na uchunguzi wa kubaini gharama za athari ya kuungua kwa moto katika moja ya nyumba iliyopo Mkokotoni Zanzibar

Rc Ayoub ameeleza hayo alivyoongoza ujumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo kumifariji familia ya wahanga wa ajali ya moto ya kuunguliwa kwa nyumba yao Febuari 6, mwaka huu huko Shehia ya Mkokotoni

Ayoub amesema serikali inaendelea kuwa karibu ili kufatilia kiini cha tukio hilo na athari zilizojitokeza ili kuchukua hatua stahiki kwa wahanga hao

Kwa upande wake mhanga wa Tukio hilo ambae ni mkaazi katika nyumba hiyo Abdallah Khamis Juma ameishukuru serikali ya mkoa kwa kufika na kuwafariji ambapo amesema moto huo umeteketeza vitu vyote katika nyumba hiyo.

View this post on Instagram

A post shared by Wasafi FM (@wasafifm)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live