Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhagama, mbunge watoa mashuka 150

Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mirerani. Mbunge wa viti maalumu (CCM), Martha Umbullah amekabidhi mashuka 150 kwa Kituo cha afya Mirerani wilayani Simanjiro.

Akikabidhi msaada huo juzi, Umbullah alisema ametoa mashuka 50 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), Jenista Mhagama ametoa 100 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mei.

Mbunge huyo alimshukuru Rais John Magufuli kwa kutekeleza ahadi ya kupeleka gari la wagonjwa na kufanikisha mradi wa maji.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mirerani, Adam Kobelo alisema gari la wagonjwa limekuwa msaada kwa wananchi wa eneo hilo kwa kuwa husafirisha wagonjwa kwenda hospitali za rufaa za KCMC mkoani Kilimanjaro na Mount Meru ya Arusha.

Naye mwenyekiti wa UWT kata ya Endiamtu, Claudia Dengesi alimpongeza waziri Mhagama na Umbullah kwa kutimiza ahadi walizotoa.

Chanzo: mwananchi.co.tz