Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhadhiri abuni jiko linalopunguza sumu ya mkaa

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Kemia kampasi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce), Dk Dativa Shilla amesema moshi wa jiko la mkaa unazalisha sumu hatari kuliko moshi wa kuni.

Akizungumza leo Julai 10 katika maonyesho ya 42 ya kimataifa ya Biashara (Sabasaba) Dk Dativa amesema alifanya utafiti mwaka 2017 na kubaini kuwa moshi wa jiko la mkaa unazalisha kemikali zenye sumu aina nne ikiwamo hewa ya ukaa.

Kutokana na kuzalisha sumu kali na kuchafua mazingira Dk Dativa aliamua kubuni majiko yanayozuia kuzalisha sumu hizo kwa wingi na kuchafua mazingira ambayo yanatumia mkaa kidogo na chuma.

“Nimetengeneza jiko hili ambalo lina chuma ndani yake, jiko linatumia mkaa kidogo na lina uwezo wa kunyonya sumu,” amesema.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz