Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgomo wa daladala Moshi waingia siku ya 7

47451 Abiriapic

Wed, 20 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Wakazi wa kata ya Msaranga wakiwemo wanafunzi katika Manispaa ya Moshi, Kilimanjaro wanalazimika kutembea mwendo wa zaidi ya kilomita mbili kutafuta usafiri wa bajaji kutokana na mgomo wa daladala unaoendelea.

Mgomo huo ulianza Jumatano iliyopita ya Machi 13, 2019 baada ya madereva wa daladala kupinga bajaji kupakia abiria kwenye vituo vyao, hivyo kugomea manispaa hiyo kulipa ushuru wa maegesho wa Sh1,000.

Wakizungumza na Mwananchi leo Jumanne Machi 19, 2019 wananchi hao wameeleza kukerwa na adha hiyo ya usafiri ambayo imedumu kwa siku saba na kusema wanachelewa kufika kazini kwa muda hali ambayo inawahatarishia vibarua vyao kupotea.

Irene Tarimo, mmoja wa wafanyakazi katika moja ya migahawa mjini Moshi ameiambia Mwananchi kuwa jana Jumatatu aliponea chupuchupu kufukuzwa kazi na bosi wake kutokana na kuchelewa mara nyingi kufika kazini kwa muda unaotakiwa.

"Mgomo huu kwa kweli umekua pigo kwetu, maana kila siku nachelewa kufika kazini kwa muda na jana kidogo bosi wangu angenirudisha nyumbani," amesema Irene.

Naye mmoja wa wanafunzi katika Shule ya Majengo, Jenifa Thomas ameeleza kutokana na tatizo la usafiri anafika shuleni akiwa amechelewa na kupelekea kukosa baadhi ya vipindi.

"Mwendo wa kutoka Msaranga hadi kufika Majengo ni mwendo mrefu, saa nyingine japo najitahidi kuwahi kuamka na kuanza safari ya shule mara nyingi nachelewa na vipindi saa nyingine nakuta vimeshaanza," amesema Jenifa.

Mgomo wa daladala Moshi kama kawaida, abiria wasota



Chanzo: mwananchi.co.tz