Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgomo wa daladala Mbeya wamalizika

Wed, 20 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mabasi yanayobeba abiria (daladala) yameanza kutoa huduma ya usafiri jijini Mbeya mchana wa leo Jumanne Machi 19, 2019 kufuatia tamko la Serikali lililotolewa katika Stendi ya Daladala Kabwe.

Mgomo huo ulioanza mapema jana Jumatatu ulikuja baada ya madereva daladala kulalamikia pikipiki za magurudumu matatu (bajaji) kufanya kazi kibiashara kwenye barabara kuu.

Mgomo huo ulihusisha daladala zote zinazobeba abiria jijini hapa na kusababisha usumbufu mkubwa ikiwemo kupanda kwa nauli kutoka Sh500 hadi 1,000 kwa bajaji na Sh3,000 hadi Sh5,000 kwa pikipiki.

Akizungumza na mkuu wa wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika amesema baada ya tamko la Serikali lililotokana na kikao kilichofanyika jana kati ya pande zinazovutana, madereva daladala wameridhia kurejesha huduma ya usafiri.

"Tulichotoa ni makubaliano ya jana kwamba watu wa bajaji na daladala walikaa na kukubaliana, hivyo daladala wamekubali kuendelea kutoa huduma na hivi ninavyoongea huduma ya usafiri imeanza," amesema.

Naye ofisa mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchikavu na Majini (Sumatra) Denis Daudi amesema kilichokuwa kinasubiriwa ni tamko la Serikali ambalo mchana huu limetolewa stendi mbele ya wahusika hivyo huduma ya usafiri imesharejea.

Kikao cha jana Jumatatu kati ya Sumatra, madereva wa daladala na madereva bajaji kilichoongozwa na Ntinika kiliamua mambo mengi ikiwemo bajaji kuacha kutumia barabara kuu kibiashara.

Pamoja na mambo mengine bajaji zilitakiwa kubeba abiria wasiozidi watatu na kuchora mistari itakayotambulisha 'ruti' ya bajaji husika.



Chanzo: mwananchi.co.tz