Mbeya. Wananchi wa Jiji la Mbeya kwa mara nyingine wamekumbana na adha ya usafiri kukufuatia mgomo wa daladala ulioanza mapema leo asubuhi Jumatatu Machi 18, 2019.
Baadhi ya wananchi wamesema mgomo huo umewaathiri kutokana na nauli kupanda kutoka Sh500 kwa pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj) na kuwa Sh1,000.
Hussein Juma amesema yeye anafanya biashara Mbalizi lakini amechelewa kutokana na kukosa usafiri na nauli kuwa juu.
"Mgomo umetuathiri sana badala ya kulipia Sh450 kwa daladala nalazimika kulipia Sh 1000," amesema.
Ibrahim Chaula ambaye ni msafiri pia amesema wameathirika kwa sababu mgomo huo umesababisha mambo yao kuchelewa na mengine kukwama kabisa.
Soma zaidi: Daladala Mbeya zagoma, abiria wasota
Related Content
Jacob Muhule mkazi wa Sae amesema mgomo umekuwa na changamoto nyingi na kuomba Serikali kutatua tatizo hili kwa haraka kwa kuwa linawakwamisha kimaendeleo.Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachojiri zaidi