Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgomo daladala Dodoma wazua balaa

Daladala Pic Data Mgomo daladala Dodoma wazua balaa

Wed, 26 Jan 2022 Chanzo: mwananchidigital

Madereva wa daladala zinazotumia kituo cha Sabasaba jijini Dodoma wamegoma kupeleka magari katika kituo hicho kutokana na kujaa kwa tope zilizosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.   Tangu daladala kuhamishiwa katika kituo hicho kila mwaka wakati wa mvua kumekuwa na migomo inayosababishwa na kuharibika kwa kituo.

Mapema asubuhi leo Jumatano Januari 26, 2022 madereva wa daladala hizo walihamishia magari yao katika eneo la bohari ambapo magari hayo yalipakia na kupeleka abiria lakini kulikuwa hakuna daladala zilizokuwa zikirejea kituoni hapo.

Hatua hiyo ilisababisha msongamano wa watu katika kituo hicho huku wengine wakiamua kupanda bajaji na pikipiki zilizokuwa zimeegesha katika eneo hilo la Bohari karibu na Stendi ya mabasi ya Kimbinyiko.

Mmoja wa madereva wa daladala, Hamis Nyange amesema wamegoma kuingia katika kituo hicho kutokana na changamoto ya ubovu, kujaa kwa matoroli na wafanyabiashara wanaochoma mishikaki jioni ambao wanahatarisha afya zao.

“Hawa wachoma mishikaki katika stendi na magari yanatumia mafuta inamaana siku yakilipuka itakuwa changamoto kwa mwenye gari anaweza kupekekwa mahakamani kwa kosa ambalo sio lake,” amesema.

Mmoja wa abiria Dometria Godfrey amesema tatizo ya kituo cha daladala ni watu kufanya biashara katika maeneo yanayoegeshwa magari na hivyo kusababisha msongamano mkubwa.

Ameoomba halmashauri ya Jiji la Dodoma kutengeneza stendi ya daladala ambayo itaepusha changamoto zikiwemo za msongamano wa watu na kujaa matope.

Chanzo: mwananchidigital