Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgomo daladala Arusha wamalizika kwa masharti haya....

Daladala Arusha Mgomoo Mgomo daladala Arusha wamalizika kwa masharti haya...

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mvutano wa siku mbili hatimaye usafiri wa Daladala Mkoani Arusha umerejea kama kawaida leo Jumatano Agosti 16, 2023.

Afisa Mfawidhi wa LATRA, Joseph Michael amesema “Kilichozingatiwa ni Sera, tumewapangia vituo vipya watu wa Bajaj, tunawaondoa mjini kuwapeleka pembeni na wamekubali hilo.”

Naye, Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Bajaji Arusha, Shafii Ramadhani amesema “Baaada ya kikao cha Agosti 15, 2023 kati ya Viongozi wa Umoja wa Bajaji, LATRA na Jeshi la Polisi tumefikia uamuzi mzuri.

“Kamati imeafikiana juu ya upangwaji wa vituo, tumefanya zoezi la kugawa Bajaji ambazo zinatakiwa kukaa kwenye vituo husika, tunashirikiana na Jeshi la Polisi na LATRA, kilichobaki kwa sasa ni nguvu kubwa kuelekezwa kwenye utekelezaji, kilichobaki ni Serikali kutoa maelekezo rasmi ya mgawanyo ndani ya wiki moja kutoka sasa.

“Pia Bajaji ambazo itapata mgawanyo wa vituo ni zile ambazo zimekidhi vigezo vya Leseni na zipo hai.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live