Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea ahakikisha ujenzi mabanda soko la Sanya

86e4e8e4997bff2e00198670b899eaee Mgombea ahakikisha ujenzi mabanda soko la Sanya

Fri, 16 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA udiwani wa Kata ya Sanya Juu wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Juma Jani (CCM) amesema endapo atachaguliwa atahakikisha ujenzi wa mabanda katika soko la Sanya unakamilika ili wananchi wafanye biashara kwa amani.

Aidha alisema atahakikisha anaunganisha umeme kwenye soko hilo ili biashara zifanyike nyakati zote. Jani alitoa ahadi hiyo wakati wa muendelezo wa mikutano yake ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo, uliofanyika katika viwanja vya Rex Sanya juu.

Alisema ameshaanza ujenzi wa mabanda na tayari amejenga mabanda mawili ambayo yana vizimba zaidi ya 16 lakini havitoshi, hivyo anaomba wananchi wamchague ili aweze kumalizia mradi huo.

“Naomba mnichague ili katika kipindi cha mwaka 2020/25 tuongeze mabanda mengine, mama zetu na wafanyabiashara wote wafanye biashara zao katika eneo hili kwa usalama hasa kipindi cha mvua,” alisema.

Aidha alisema atahakikisha anaweka umeme kwenye soko hilo ili wafanyabiashara wafanye biashara zao hadi nyakati za usiku na kulifanya soko hilo kuwa la kila siku kama masoko mengine na kuongeza ajira.

Katibu wa CCM wilaya, Mwaisha Mbisha alitaka wananchi kulinda kadi zao za kupigia kura ili waweze kuwa na sifa na kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka.

Chanzo: habarileo.co.tz