Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mghwira atoa onyo kwa wazazi

50d43b582039f1fa0f7ed03915e32821 Mghwira atoa onyo kwa wazazi

Thu, 14 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema serikali haitamvumilia mzazi yoyote atakayeacha kumpeleka mtoto wake mwenye sifa ya kujiunga shule ya awali au darasa la kwanza au kidato cha kwanza, mwaka huu.

Amesema hayo jana mkoani humo na kusisitiza kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule kwa ajili ya elimu ya awali na darasa la kwanza wakaandikishwe na kuanza masomo mara moja.

Aidha, amesisitiza kuwa wanafunzi wote waliofaulu na kuchaguliwa na kujiunga na elimu ya sekondari, wadahiliwe na kuanza masomo yao haraka iwezekanavyo.

Amewaelekeza wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye sifa ameandikishwa na anaenda shule.

Chanzo: habarileo.co.tz