Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mghwira ashauri wajasiriamali kutumia benki kupata mikopo

9ac69b1ca878935d36dcb8da6c684b25 Mghwira ashauri wajasiriamali kutumia benki kupata mikopo

Sun, 4 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ametoa rai kwa wajasiriamali nchini kutumia fursa za benki kwa ajili ya kupata mikopo na kupata mbinu za kupata masoko nje ya nchini

Mghwira aliyasema hayo jana wakati alipofungua kongamano la wajasiriamali lililoanza juzi na linatarajiwa kumalizika keshokutwa.

Alisema wanawake wengi wanapenda kujikwamua kiuchumi kwa kutumia fursa za kibiashara kwa kubuni ujasiriamali wa aina mbalimbali hivyo kupitia kongamano hilo wanaweza kujifunza na kujadili changamoto za kibiashara ili kujikwamua kiuchumi.

“Wanawake wanajikwamua kiuchumi kwa kubuni miradi mbalimbali ya kimaendeleo hivyo ni lazima mjue changamoto hazikosekani lakini nawasihi pamoja na changamoto lazima mjue mnajukumu kubwa la kulea familia zenu,” alisema.

Alitoa rai kwa wanawake kuchagua viongozi sahihi haswa kipindi hiki cha uchaguzi ili wagombea hao waweze kusema changamoto wanazokumbana nazo wajasiriamali na kusisitiza zinapotokea fursa za uongozi za kugombea au kuteuliwa lazima wahusika wajue umuhimu wa wanawake katika kuleta maendeleo.

Mwandaaji wa kongomano hilo, Gladness Katega alisema kongamano hilo litawasaidia wanawake wa Tanzania kuinuka kiuchumi na kutanua biashara zao ikiwa lengo lao ni kuona wanawake wakifanya biashara kwa pamoja kupitia ushirikiano na umoja wao.

Kongamano hilo limedhaminiwa na wadau mbalimbali na wanawake kutoka nchi mbalimbali zaidi ya 90 wanashiriki.

Chanzo: habarileo.co.tz