Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mghwira: Wafanyabiashara kuweni wabunifu

67840 Pic+mgwira

Mon, 22 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amewataka wafanyabiashara mkoani humo kuwa wabunifu na kujenga hoja zenye nguvu pindi kunapoibua changamoto na vikwazo kwenye biashara zao.

Mghwira ametoa rai hiyo leo Jumatatu Julai 22,2019,wakati akifungua kikao cha wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kilichokuwa na lengo la kusikiliza kero, changamoto, maoni na ushauri kutoka kwa wafanyabiashara.

Amesema suala la wafanyabiashara kulipa kodi ni la lazima hivyo ni jukumu la wafanyabiashara kuwa wabunifu na wenye uthubutu ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuongeza makusanyo ya kodi na kuufikia uchumi wa viwanda.

"Wafanyabiashara ongezeni nguvu na ubunifu, kunapoibuka changamoto au vikwazo, jengeni hoja zenye nguvu na acheni woga,  hiyo itasaidia kutengeneza mnyororo wa faida,"amesema Mghwira.

Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Msafiri Mbibo amewataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo, kutosheka na mishahara yao na kuepuka kujihusisha na vitendo vya rushwa.

 

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz