Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgawo wa maji Mtwara siku 60

60357 Pic+mtwara

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Wakazi wa mji wa Mtwara watalazimika kupata huduma ya maji kwa mgawo kwa muda wa miezi miwili kutokana na ujenzi wa barabara unaoendelea kwa kiwango cha lami.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Mei 29, 2019  mwakilishi wa mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Mtwara, Sauna Keya amesema mgawo huo utakuwa zaidi ya uliopo sasa kutokana na ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba–Newala hadi Masasi.

Amesema kutokana na ujenzi huo, wanalazimika kuhamisha miundombinu ya maji.

Amebainisha kuwa kuondolewa kwa miundombinu kutaathiri  huduma ya upatikanaji wa maji na mamlaka hiyo inahakikisha ukosekanaji wa maji hauwi asilimia 100 kwa kutengeneza bomba la dharura yatakayosaidia maji kupatikana wakati miundombinu ikihamishwa.

“Bomba letu kubwa linaloleta maji maeneo yote ya mjini lipo kwenye barabara hiyo na bahati nzuri mamlaka imeshalipwa fedha za kuondoa miundombinu yake katika barabara hiyo na kinachofuatia sasa ni utekelezaji,” amesema Sauna.

Meneja wa mradi huo, Ramadhan Chubi kuna wakati watalazimika kuzuia maji ili kufanya matengenezo jambo mpaka Julai mgawo huo utapungua.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz