Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgao wa Umeme tena kwa saa 12

Tanesco.jpeg Mgao wa Umeme masaa 12, Rukwa

Sat, 19 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Umeme (TANESCO ) Mkoa wa Rukwa limetoa taarifa ya kukatika kwa umeme siku ya kesho Jumapili, Februari 20, 2022 ambapo huduma ya umeme haitakuwepo kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 1:00 usiku.

Sababu itakayopelekea kukatika kwa umeme ni kupisha matengenezo katika kituo cha kupooza na kusambaza umeme –Mbala nchini Zambia.

Maeneo yatakayo athirika ni baadhi ya maeneo ya Maeneo ya Sumbawanga mjini, Wilaya yote ya kalambo, Wilaya yote ya laela, wilaya yote ya Nkasi na Halmashauri ya Mpimbwe.

"TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, tafadhali usishike wala kukanyaga waya ulioanguka..."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live