Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgao wa Maji wamalizika Chalinze

Jen Mwam Jenerali Mwamunyange akiwa na Mtendaji Mkuu wa Dawasa

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na mgao wa maji uliokuwepo kwa wakazi wa Chalinze, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) sasa imehitimisha changamoto hiyo ya muda mrefu ya maji.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa maji wa Mlandizi - Chalinze - Mboga Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa Chalinze na maeneo ya karibu kupata majisafi kwani mradi huo umekamilika hivyo amewataka wananchi kwenda kwenye ofisi za Mamlaka hiyo ili kuweza kujisajili kwa ajili ya kupatiwa huduma ya maji ili kutimiza lengo la Rais Samia la kumtua Mama ndoo kichwani.

"Leo nimekuja na wajumbe wa Bodi ili kujihakikishia kama kweli zile fedha tunazozihidhinisha kama kweli zinahakisi kilichopo kwenye miradi husika" alisema Mwamunyange

Pia Mwamunyange amesema Bodi imefuatilia na kukagua uchimbaji, ulazaji wa Bomba pamoja na ujengaji wa Pampu za kusukumia maji na wamejiridhisha mradi huo umekamilika kwa asilimia mia hivyo imebaki kazi ya wananchi kuanza kutumia maji ya mradi huo.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Mradi wa Maji wa Ruvu Juu hadi Mboga ni Mradi unaenda kuondoa kero ya upatikanaji wa Maji katika maeneo ya Mlandizi, Chalinze na Mji Mdogo wa Mboga, pia Mradi huu umelaza mabomba ya inchi 12 kwa umbali wa Kilomita 59 kutoka mtambo ya Ruvu Juu hadi Chalinze, Mji wa Mboga.

Pia amesema kiasi cha Shilingi Bilioni 18 kimetumika kwenye Miradi wa Maji wa Ruvu Juu mpaka Msoga itakayotatua kero ya Maji kwa wananchi zaidi ya 122,000 wa maeneo hayo hivyo kumalizika kwake itakuwa ndio suluhu la upatikanaji wa maji kwenye mji wa Chalinze, Pingo, Pera, Msoga, Bwilingu, Msata, Kihangaiko, na Ubenazimozi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live