Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mganga wa kienyeji alia kutapeliwa Mbeya

Mganga Wa Kienyeji Alia Kutapeliwa Mbeya Mganga wa kienyeji alia kutapeliwa Mbeya

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyo ya kawaida Mganga wa kienyeji Edward Mwansasu mkazi wa Kijiji Cha Ndubi Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya, amefika mbele ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya kulalamika juu ya kutapeliwa na mteje wake aliye mhudumia kwa kumpa dawa za biashara.

Mganga huyo amefika mbele ya mkuu wa Mkoa wakati akisikiliza kero za wananchi Wilayani humo akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali na kusikiliza kero za wananchi ambapo mbali na hilo amelalamikia hatua ya wazee na walemavu katika Kijiji cha Ndubi kutopata misaada inayo tolewa na serikali ikiwemo vyerehani na fedha za tasaf.

Akijibu malalamiko hayo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera ameelekeza wataalamu kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, kufika katika Kijiji hicho Ili kuangalia namna ya kuwawezesha walemavu na wazee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live