Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgalu: Umeme ukitumika vyema huchochea maendeleo

28686 Umeme+pic TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pwani. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wakazi wa Jaribu Magharibi mkoani Pwani kuitumia nishati ya umeme kukuza uchumi  na kuboresha elimu kwa watoto wao.

 

Mgalu ameyasema hayo leo Novemba 24, 2018 wakati akizindua utumiaji wa nishati ya umeme katika nyumba 22 zilizopo eneo hilo zilizounganishwa kupitia mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) awamu ya tatu.

 

Mgalu amesema nishati ya umeme ni chanzo cha maendeleo katika kila sekta,  endapo itatumiwa ipasavyo huchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi.

 

"Tunataka tuone mabadiliko katika elimu, huduma za afya, biashara na ajira kwa sababu hakuna kikwazo cha kuwafanya mshindwe kutekeleza hayo yote," amesema Mgalu.

 

Awali akizungumzia mradi huo mhandisi mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Pwani, Suleimani Mgwira amesema licha ya kuwa kaya 22 zimenufaika na umeme huo katika awamu ya kwanza lakini wanaendelea na uhamasishaji ili watu wengi waweze kunufaika.

 

"Mradi huu umejengwa kwa urefu wa kilomita 2 kwa njia kubwa na kilomita 1.8 njia mdogo hivyo ni matumaini yangu watu wengi bado wanayo fursa ya kunufaika na mradi huu," amesema Mgwira.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz