Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfumo wa kujikwamua kiuchumi wazinduliwa Dar

46395 PIC+KIJIKWAMUA Mfumo wa kujikwamua kiuchumi wazinduliwa Dar

Wed, 13 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tume ya Sayansi na Technolojia (Costech) imezindua mfumo mpya wa  Mafunzo ya Ujasiriamali kwa njia ya Kidijitali (BESP) wenye lengo la kuwasaidia wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi.

Mfumo huo umezinduliwa leo Jumanne Machi 12,2019 na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sita katika ofisi za Costech jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kuzindua mfumo huo Sitta amesema utakwenda kutatua changamoto za ajira kwa vijana kwa kuwa unatoa fursa ya kujiajiri wenyewe.

“Tunaishukuru Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) kwa kuanzisha mfumo huu ambao sasa vijana hawatalalamika tena kuhusu ajira, kwani watajifunza mbinu mbalimbali za kijasiriamali pamoja na ubunifu katika biashara,” amasema.

Naye Mkurugenzi Mkuu Costech, Amos Nungu amesema ili kujenga uchumi wa nchi vijana wanatakiwa kupewa mbinu mbalimbali itakayowawezesha kujifunza, kujiajiri na kuajiri wengine.

“Mimi nitoe wito kwa vijana kuchangamkia fursa hii na kujisajili kwa ajili ya kupata mafunzo ambayo yanatolewa kwa njia ya mitandao kupitia kompyuta na simu za mkononi,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz