Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyakazi ofisi ya DC afariki kwa ajali ya gari

Ajali Godwin Mfanyakazi ofisi ya DC afariki kwa ajali ya gari

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mfanyakazi wa kujitolea katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Maxmillian Godwin amefariki kutokana na ajali ya gari.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya amethibitisha habari hizo na kusema Godwin alipata ajali Disemba 5 mwaka huu akitokea Njombe kuelekea Songea.

Godwin ni kijana aliyeshiriki katika tuzo za Tanzania Youth Emerging Awards 2022 na kushinda kipengele cha Kupambana na Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele (Outstanding Youth in Health-care Advocacy).

Kyobya amesema Godwin alikuwa anasoma Ufamasia katika Chuo Kikuu cha Zambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live