Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara akutwa amekufa kwenye gari lake

Gari Mslsls.jpeg Mfanyabiashara akutwa amekufa kwenye gari lake

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwili wa mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Muksini, ambaye ni mfanyabiashara wa bucha umekutwa kwenye gari yake katika eneo la Uwanja wa Fisi Maduka 9 jijini Mwanza, akiwa amefariki huku ikisadikika kunyongwa na kamba ambayo ilikutwa ndani ya gari hiyo

Wakizungumza katika tukio hilo, baadhi ya mashuhuda wamesema  majira ya saa 2:00 asubuhi wamelikuta gari hilo likiwa kandokando mwa barabara huku mwili huo ukiwa ndani ya gari.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa, amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akisema bado uchunguzi unaendelea kufanyika ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live