Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara akutwa amejinyonga Arusha

94183 Pic+jinyonga Mfanyabiashara akutwa amejinyonga Arusha

Mon, 3 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mfanyabiashara wa Mitumba na Mkazi wa Sanawari Mtaa wa Texas jijini hapa, Kelvin Didas (26) anadaiwa kujinyonga hadi kufa eneo la jirani na nyumbani kwake.

Mke wa mfanyabiashara huyo, Jack Denis amesema mumewe hakurudi nyumbani usiku wa kuamkia  leo  Jumapili Februari 2, 2020 kutokea kazini na yeye hakushtuka maana huwa ni kawaida yake  siku zingine kutorudi   nyumbani akijua wamefuata mzigo mkoani Tanga.

Akizungumza na Mwananchi, amesema mapema leo asubuhi alipata taarifa kutoka kwa jirani yake aliyefika nyumbani kwake na kumuulizia alipo mumewe naye alimjibu hajarudi tokea jana.

“Nikaambiwa nitoke nje nielekee eneo alipo, nikamkuta tayari amekufa akiwa amenyongwa na nguo zake,” amesema.

Marehemu ameacha mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la amani Kelvin (2) .

Akizungumzia tukio hilo, Balozi wa mtaa huo, Elizabeth Thimos amesema leo asubuhi Saa 2 kasoro robo alifuatwa na mama anayejulikana kwa jina la mama Winner  na kumueleza kuwa kuna mtu amekufa, akachukua hatua ya kumtafuta mwenyekiti wa kitongoji hicho lakini hakupatikana  .

Pia Soma

Advertisement
Balozi aliendelea kusema baada kutompata kiongozi mwenzake ndipo alipochukua hatua ya kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Mjini kati ambao walifika na kuuchukua  mwili kwa ajili ya uchunguzi zaidi pamoja na kuuhifadhi.

Hata hivyo, haijulikani kama marehemu alijinyonga mwenyewe ama amenyongwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha, Jonathan Shana amethibitisha kupata taarifa za tukio hilo na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Chanzo: mwananchi.co.tz