Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meya na wenzie kizimbani kwa uhujumu uchumi Tanga

Rushwa Tanzania Meya na wenzie kizimbani kwa uhujumu uchumi Tanga

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustafa Seleboss na wenzake watano, Omari Ali Salehe, Amina Rajab Mbwana, Pilly Salum Shomari, Mwajuma Sabdallah Mwaimu na Mwanakondo Kichui Mwalimu wamepandishwa kizimbani kwa makosa manne ikiwemo kughushi nyaraka na kujipatia pesa isivyo halali.

Makosa hayo ni ya kugushi Barua ya maombi ya kufungua akaunti ya Benki ya NMB kwaajili ya mkopo wa kikundi, wizi wa Tsh milioni 5 ya Halmashauri ya jiji la Tanga, matumizi mabaya ya madaraka ya ya umma na kusababisha hasara kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Joseph Mulebya mbele ya Hakimu wa Mahakama ya ya Hakimu Mkazi, Suniva Joseph Mwajombe amesema kati ya mei 28 /2019 na Mei 2022 Washtakiwa walifanya makosa hayo kwa makusudi hali wakijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Mulyeba amesema, watuhumiwa hao kwa pamoja walighushi nyaraka mbalimbali kwa ajili ya kujiaptia Tsh milioni 5 ambazo fedha za umma zinazotolewa na Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 za vijana,wanawake na maku ndi ya wenye ulemavu.

Kwa upande wake Selebosi, Mwendesha mashtaka huyo alisema anashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa fedha za umma kinyume na sheria ya matumizi ya madaraka.

Washtakiwa wengine, wamefikishwa mahakamani hapo kwa madai ya kuisababishi hasara ya Tsh milioni 5 Halmashauri ya Jiji la Tanga, na kesi hiyo namba saba ya mwaka 2023 imeahirishwa hadi Juni 20, 2023 kwa ajili ya kutajwa tena na washtakiwa wote wamerejeshwa rumande kutokana kwa kukosa wadhamini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live