Meya wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Godson Gypson ametoa siku tatu kwa Mkuu wa shule ya sekondari Buhembe Constantine Nyawawa kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika
Meya huyo pia amemuagiza Ofisa elimu sekondari Frances Nshaija kufuatilia ili kubaini kama kuna uzembe umefanyika katika ujenzi na kuchukua hatua.
Gypson ametoa maagizo hayo jana Ijumaa, Desemba 10, 2021 katika ziara na madiwani wenzake kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa 30 katika kata 14 za Manispaa ya Bukoba vinavyojengwa kwa Sh600 milioni ambazo ni fedha za Uviko-19 zilizotolewa na Serikali.
Madiwani Manispaa ya Bukoba baada ya kufika kata ya Buhembe hakuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na hivyo Meya Gypson akatoa siku tatu kwa mkuu wa shule hiyo kuhakikisha anasimamia ujenzi huo na unakamilika kwa muda uliopangwa.
Ofisa elimu sekondari Manispaa ya Bukoba France Nshaija amesema kuwa, shule ya sekondari Buhembe bado iko kiwango cha chini cha ujenzi kati ya 50 hadi 60 asilimia huku sekondari nyingine zikiwa hatua ya umaliziaji kati ya 85 hadi 90 asilimia.
Amesema hata hapo ujenzi ulipofikia idara ya yake imekuwa akifanya ukaguzi wa mara kwa mara na ataendelelea kufanya hivyo ili ujenzi ukamilike kwa wakati katika shule hiyo.
Advertisement Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Constantine Nyawawa amesema kuchelewa kwa ujenzi kumesababishwa na kubadilisha mzabuni kwakuwa aliyekuwapo alishindwa kuleta vifaa kwa wakati.
Ikumbukwe kuwa kila chumba moja ya darasa kinajengwa kwa Sh20 milioni na kwa mkoa wa Kagera ujenzi umeanza Novemba mosi, mwaka huu ulipaswa kukamilika Novemba 30, mwaka huu kwa maagizo ya Mkuu wa Meja Generali Charles Mbuge.