Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meya ang’aka kuongezeka kwa matukio ya ukatili kwa watoto

Ukatili Watoto Meya ang’aka kuongezeka kwa matukio ya ukatili kwa watoto

Tue, 20 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada ameng’aka juu ya kuongezeka kwa matukio ya kikatili dhidi ya watoto hasa ubakaji, ulawiti na vipigo.

Hivi karibuni Ngwada alinukuliwa akisema kuna moja kati ya shule za msingi ambazo zaidi ya watoto 20 wamefanyiwa ulawiti jambo ambalo ni hatari.

Mwanzoni mwa mwaka huu, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 alitiwa mbaroni kwa tuhuma za kuwalawiti wenzake 19, katika eneo la Kihesa Kilolo, Manispaa ya Iringa.

Akizungumza leo Desemba 20 mkoani hapoa, Ngwada amesema haiwezekani watoto wakaendelea kuumizwa wakati wanaishi kwenye jamii yenye wazazi, walezi, walimu, viongozi wa dini na Serikali.

“Haiwezekani watoto wakaendelea kufanyiwa ukatili wa aina hii wakati sisi tupo, kwanini matukio haya yanatokea? Nataka kila mmoja ajiulize maswali haya. Hii sio sahihi kabisa, tunatengeneza kizazi cha ajabu kabisa,” amesema Ngwada.

Amewataka wazazi na walezi kuwa makini kwa kuwajali na kuwalinda watoto wao wakati wanapokuwa nyumbani.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego alisema ulevi kupindukia, imani potofu na kulegea kwa malezi ya watoto vinachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa vitendo vya ukatili kwa watoto katika mkoa huo. Amesema Iringa bila ukatili wa kijinsia inawezekana ikiwa kila mmoja wetu atatimiza wajibu wake ipasavyo.

Amelitaka Jeshi la Polisi kuweka kufanikisha upelelezi ili kuwezesha mahakama kuchukua hatua. 'Naagiza kila halmashauri kutoa elimu kwenye mitaa, kata na Vijijini mashuleni ili wananchi wawe na uelewa mpana kuhusu masuala hayo alisema Dendego,” alisema Dendego.

Afisa Ustawi wa Jamii Manisaa ya Iringa, Tiniel Mbaga alisema juhudi za kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia zimekuwa zikifanywakwa ushirikiano baina ya halmashauri, taasisi za dini, vyombo vya habari na taasisi zisizo za kiserikali.

Chanzo: Mwananchi