Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meya aagiza Milioni 3.2 za kununua bastola ya Mkurugenzi zirudishwe

Glok 29 Pistolet Oruzhie Oboi 660x400.jpeg Meya aagiza Milioni 3.2 za kununua bastola ya Mkurugenzi zirudishwe

Sat, 29 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Meya wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza Milioni 3.2 zilizotengwa na Halmashauri ya Manispaa hiyo kwa ajili ya kununua bastola ya Mkurugenzi zirejeshwe.

Raibu ametoa tamko hilo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Stephen Kagaigai ambaye pia alishiriki kikao hicho.

Amesema fedha hizo zilipitishwa na halmashauri hiyo mwaka 2015 na kubainisha kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

“Kuna fedha zilipitishwa mwaka 2015 kiasi cha Sh3.2 Milioni kwenye akaunti ya Halmashauri kununua bastola ya Mkurugenzi, haya  ni matumizi mabaya ya fedha za umma, nimeagiza fedha hizi zirudishwe mara moja,” Raibu.

DIAMOND PLATNUMZ ATINGA OFISI ZA CCM, “NIMEFARIJIKA KUONA RAIS SAMIA KAAMINI VIJANA”

Chanzo: millardayo.com