Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meya Tanga atoa wiki tatu marekebisho majengo

Jengo La Karakana.jpeg Meya Tanga atoa wiki tatu marekebisho majengo

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meya wa Jiji la Tanga, Abdurhaman Shillow, ametoa muda wa wiki tatu kwa wamiliki wa majengo mabovu, machafu yaliyochoka katikati ya Jiji hilo na kuharibu taswira kuhakikisha yanafanyiwa uwekezaji, yarekebishwe ili yaendane na hadhi ya mji huo.

Alitoa kauli hiyo juzi wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha robo ya pili ya mwaka wa fedha ya 2022/2023 ambapo alisema wamejipanga kuhakikisha mji huo unakuwa na mwonekano mzuri.

Shillow alisema haiwezekani kuwapo kwa nyumba, majengo mabovu na machafu ambayo yanaweza kusababisha kuondoa mandhari na hadhi ya Jiji hilo.

"Kwa hiyo kuanzia leo natoa muda wa wiki tatu kwa wamiliki wa majengo mabovu, machafu yaliyochoka katika ya Jiji hilo kuhakikisha yanafanyiwa uwekezaji, yarekebishwe au yauzwe kuendana na hadhi ya mji huo," alisema.

Aidha, alimpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Sh. milioni 580 kwa ajili ya kuondoa adha ya wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza ili kukabiliana na uhaba wa madarasa.

Hata hivyo, aliwataka wafanyabiashara wanaofanya biashara kwenye barabara zisizokuwa na matumizi hayo na kuleta uhatarishi kwenye vyombo vya moto na watumiaji wa miguuu waache mara moja kufanya biashara kwenye maeneo hayo ikiwamo kutoka nje kwenye maduka yao na kupanga barabarani.

Pia alimtaka Mkurugenzi wa Jiji hilo na watumishi wengine wahakikishe wanalisimamia suala hilo ili kuweza kuidhibiti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live