Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meya Dar azuiwa kuingia ofisini

91648 Pic+meya Meya Dar azuiwa kuingia ofisini

Mon, 13 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita leo asubuhi amefika ofisini kwake katika jengo la Karimjee ili aendelee na majukumu yake ya kila siku.

Hata hivyo katika hali ambayo pengine hakuitarajia, alikuta mlango wa ofisi yake umebadilishwa nywila ya kuingilia hali iliyomlazimu kusubiri nje ya ofisi hiyo.

Akizungumza na MCL, Mwita amesema kufuatia hali hiyo hawezi kuingia ndani mpaka atakapojiridhisha.

Katika hali ya kushangaza walinzi waliokuwepo eneo hilo walikuwa wakizuia mtu yeyote kuingia katika ukumbi huo kwa maelekezo kuwa mpaka wapate kibali kutoka juu.

Pia wakati waandishi wakiondoka eneo hilo walimshuhudia diwani wa Tabata, Patrick Asenga naye akizuiwa kuingia.

Kwa Taarifa Zaidi endelea kusoma Mwananchi na kufuatilia mitandao yetu

Chanzo: mwananchi.co.tz