Wananchi wa Ikombe kata ya Matema wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya wamemkabidhi Meneja wa TANESCO wilayani humo Kibatali ikiwa ni ishara ya kuachana na matumizi ya mafuta ya taa na umeme wa wa jua baada ya kufikiwa na umeme wa gridi ya taifa kupitia mradi usambazaji Umeme Vijijini REA.
"Ulivyofika umeme matarajio yetu kutakuwa na biasahara nyingi katika kijiji chetu cha Ikombe maana umeme ndo kila kitu kwa ajili biashara watu watakuwa na saloon" - Imani Makolo, Mkazi wa Ikombe.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase amewataka wananchi kutunza miundombinu lakini kutumia nishati ya umeme kujiletea maendeleo.