Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meli kubwa za kubeba mizigo, abiria kuanza ziwa Nyansa

89851 Meli+pic Meli kubwa za kubeba mizigo, abiria kuanza ziwa Nyansa

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Watumiaji wa ziwa Nyasa nchini Tanzania kuanzia Januari mwaka  2020 kiu yao itapona baada ya meli kubwa ya kubeba mizigo na abiria (MV Mbeya 2) itakapoanza kufanya safari katika ziwa hilo ambalo lipo mpakani mwa nchi za Tanzania, Malawi na Msumbiji.

Hivi sasa ambapo meli hiyo haijaanza kutumika wakazi wa maeneo ya ziwa hilo ambalo limezungukwa na milima ya Livingstione hutumia mitumbwi kutoka sehemu moja kwenda nyingine jambo ambalo linaelezwa sio salama kutokana na ukubwa wa mawimbi.

MV Mbeya 2 ambayo imeundwa kwa gharama ya Sh9.1 bilioni ina uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mzigo, hivi sasa ipo katika majaribio ya mwisho ili kupewa vibali vya kuanza kutumika kwake.

Meneja wa bandari za ziwa Nyasa, Abeid Galus anasema meli hiyo ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kuwa na meli tatu katika ziwa hilo ambapo tayari mbili zenye uwezo wa kubeba tani 1000 kila mmoja zilikamilika na kuanza kutumika tangu 2017.

“TPA shughuli zake ni za bandari tu lakini katika ziwa Nyasa ililazimika kuingia katika biashara ya meli ili kunusuru shughuli za bandari katika ziwa na kutoa suluhisho la usafiri kwa wakazi wanaozunguka ziwa hilo;” anasema Galus.

Jana Jumatatu Desemba 23, 2019 Mwananchi ilipata nafasi ya kuishuhudia meli hiyo katika eneo ilipokuwa inajengwa (Bandari ya Kiwira ambao ilishuhudia meli hiyo ikijaribiwa, jambo la kuvutia zaidi ni madhali ya ndani ya meli hiyo ambayo ndani muundo wake ni kisasa.

Viti vyake ni katika eneo la daraja la kati ni kama vya basi, daraja la juu (VIP) kuna vitanda na viti vya maliwato lakini pia mgahawa wake ni wakuvutia.

Nahodha wa meli hiyo Charles Mkumbi anasema meli hiyo ipo vizuri imeweza kwenda Matema na kurudi bandarini hapo bila shida. “uzuri wa meli hii ina uwezo wa kutia nanga mahali popote.”

Chanzo: mwananchi.co.tz