Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji atolewa vitu kwenye nyumba ya kupanga, adai kisa yeye Chadema

IMG 20220911 160309 823 681x306 Mchungaji atolewa vitu kwenye nyumba ya kupanga, adai kisa yeye Chadema

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji Frabius Mukoba wa Kanisa la Full Victory Gospel Church ambaye ni mkazi wa mtaa wa Majengo kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga ameiomba serikali kuingia kati mgogoro ambao umeibuka kwenye nyumba yake aliyopanga.

Ameyasema hayo juzi baada ya kufika mwenyekiti wa mtaa huo akimtaka kuhama kwenye chumba alichopanga ambapo ameeleza kuwa siku ya Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu, baba mwenye nyumba alimtaka kuhama kwenye chumba chake alichopanga Mchungaji Mukoba kwa kudai kuwa amepata mpangaji mwingine.

Mchungaji Mukoba ameeleza zaidi kuwa yeye ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA na kwamba inasadikika ndiyo sababu inayochochea mgogoro.

Mchungaji Frabius Mukoba wa Kanisa hilo la USHINDI ambalo lipo Masekelo kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga ameiomba serikali kuingilia kati mgogoro huo kwa kusimamia haki ili kumaliza changamoto hiyo.

“Jana (yaani Septemba 10), mwenye nyumba alikuja akanigongea akasema chumba hiki anataka kukibadilishia matumizi, kwa hiyo nihamie kwenye chumba kingine, nikamwambia basi nionyeshe hicho chumba nione kama vitu vyangu vitaenea, nilipoenda kukiona kile chumba kikawa nyavu zimetoboka toboka chini hakuna hata sakafu halafu rangi hakijapakwa kulingana na gharama ambayo mimi nalipa.

"Nikamwambia sasa mzee naona umenichoka, mimi naomba nipe muda nitafute chumba kingine nihamishe vitu vyangu lakini huwezi kuchukua hela za mtu kama umepata mpangaji mwingine wa kuongeza hela afanyie biashara kwenye chumba hiki na juzi tu nimekupa hela Tsh 60, mpaka Oktoba 1.

"Ungeniambia kwamba hizi hela usinipe nenda katafute chumba kingine lakini hela zangu umepokea na sasa hivi unaniambia nitoke kwenye chumba hiki, akaniambia kwamba yeye ni Mchaga lazima nitahama kama nikitaka kukaa kwenye chumba hicho basi niwe nalipia laki moja na nusu kwa miezi mitatu”.

“Leo Jumapili mimi natoka kwenye ibada saa sita nikamkuta mwenyekiti wa mtaa na kamati yake, mwenye nyumba hakuwepo, sijapewa hata notisi ya kuhama, mwenyekiti akaniambia kwanza wewe ni mkeleketwa wa CHADEMA hata wapangaji hawakuelewi na mwenye nyumba hakutaki kwa hiyo kuanzia sasa toa vitu vyako vyote nje na mgambo utawalipa uende unakokujua”.

“Kwa kweli hiki kilichonitokea ninaiomba serikali iliangalie kwangu na mtu mwingine tusichukulie itikadi za vyama wala kidini kwa kuleta usumbufu na kuharibu amani za watu. Kwa hiyo naiomba sana serikali inisaidie angalau nipate muda wa kutafuta sehemu ya kuweka hivi vitu vyangu pamoja na mimi ili nikae kwa Amani,” amesema Mchungaji Mukoba.

Kwa mujibu wa baba mwenye nyumba hiyo, mzee Adam John Mwanga mkazi wa kata ya Ngokolo mjini Shinyanga ambaye ameeleza changamoto zilizopo kwa mpangaji wake ambapo amesema kuwa halipi kwa wakati hela ya kodi.

“Huyu mpangaji kwanza haelewani na wapangaji wengine maana walikuja kunilalamikia, vilevile nilimwambia atoke kwenye chumba anacholala cha biashara maana kuna wapangaji wanakitaka chumba hicho wafanyie biashara.

"Akasema mizigo yangu nitaiweka wapi, ikabidi nimtafutie chumba kingine nikamwabia hiyo mizigo yako hamishia huku kama havitaenea nitakupa na chumba kingine cha pili bure lakini uachie chumba hichi cha biashara maana huu mlango ni wa biashara.

“Akasema hawezi kuhama kwenye chumba hicho, nikamwambia sasa kama unaona huwezi kuhaka kwenye hicho chumba basi ulipie bei ya hiki chumba maana wale wengine wanalipia elfu 50 kila chumba ila yeye analipia elfu 30 tu”.

“Nilienda kwa mwenyekiti wa mtaa kutoa taarifa akasema nimwachie yeye atalifanyia kazi maana huyo mchungaji mimi nimemwambia watu wanakitaka chumba hicho tayari nimeshachukua hela yao yeye anasema nimpe nafasi mpaka mwezi wa kum,” amesema Mzee Mwanga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Majengo Bwana Majid Ally naye ameeleza juu ya mgogoro huo ambapo amesema amechukua hatua hizo baada ya kupokea malaliko kutoka kwa baba mwenye nyumba pamoja na wapangaji wengine waliopo kwenye nyumba hiyo ya mzee Mwanga

“Mwenye nyumba alikuja akaeleza kuwa mpangaji wake halipi hela kwa wakati lakini pia haelewani na wapangaji wengine anatakata kumtoa kwenye chumba hicho lakini hataki hii ya kusema kwamba huyo mpagaji tumetoa vitu vyake nje siyo kweli.

“Sisi tumefika pale leo tukamwambia toa vitu vyako uhamishie kwenye chumba kingine kwa muda wakati ukiwa unatafuta chumba kingine ya kwenda kuishi na kwa matukio yako ya namna hii sisi kwenye mtaa wetu hatukuhitaji utafute sehemu zingine ukaishi akafungua milango akatoa baadhi ya vitu vyake mimi nikaondoka nikamwachia maagizo mjumbe wangu,” amesema Mwenyekiti Majid.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live